93 DUHA

 • 93:1

  Naapa kwa mchana!

 • 93:2

  Na kwa usiku unapo tanda!

 • 93:3

  Mola wako Mlezi hakukuacha, wala hakukasirika nawe.

 • 93:4

  Na bila ya shaka wakati ujao utakuwa bora kwako kuliko ulio tangulia.

 • 93:5

  Na Mola wako Mlezi atakupa mpaka uridhike.

 • 93:6

  Kwani hakukukuta yatima akakupa makaazi?

 • 93:7

  Na akakukuta umepotea akakuongoa?

 • 93:8

  Akakukuta mhitaji akakutosheleza?

 • 93:9

  Basi yatima usimwonee!

 • 93:10

  Na anaye omba au kuuliza usimkaripie!

 • 93:11

  Na neema za Mola wako Mlezi zisimlie.

Paylaş
Tweet'le